Alhamisi 18 Juni 2026 - 12:18
“Bendera ya Imam Hussein (as) Yapeperushwa Daresalam Tanzania; Majlisi za Muharram 1448H Zaanza”

Hawza/ Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Imam Swa'diq (as), Sheikh Muhammad Abdu ameongoza Hafla ya Upandishaji wa Bendera ya Imam Hussein (as) na Kuzindua Kaulimbiu ya Muharram 1448H, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Majlisi za Abiiabdillah Hussein (as).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika hali ya kiroho iliyojaa hamasa na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as), Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Imam Swa'diq (as), Sheikh Muhammad Abd, ameongoza hafla ya upandishaji wa Bendera ya Imam Hussein (as), ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa maadhimisho ya mwezi mtukufu wa Muharram 1448 Hijria, unaosadifiana na mwaka 2026, ambapo hafla hiyo ilifanyika katika mazingira ya kiroho na mshikamano, huku ikiwakutanisha viongozi wa dini, wanafunzi wa Hawza na waumini mbalimbali waliojitokeza kushiriki tukio hilo muhimu la kuadhimisha kumbukumbu ya harakati za Karbalaa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Muhammad Abdu alieleza kuwa; upandishaji wa Bendera ya Imam Hussein (as) ni nembo ya kuhuisha ujumbe wa milele wa Karbalaa na kuwakumbusha Waislamu pamoja na wapenda haki duniani kote kuhusu misingi ya uadilifu, uhuru, kujitolea na mapambano dhidi ya dhulma ambayo Imam Hussein (as) aliitetea kwa ujasiri na msimamo usioyumba.

Alisisitiza kuwa; mwezi wa Muharram ni fursa adhimu ya kurejea mafunzo ya tukio la Karbalaa, kujijenga kiroho na kimaadili, pamoja na kuimarisha mshikamano wa Kiislamu na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as), ambao walitoa mfano bora wa kusimamia haki na kutetea utu wa mwanadamu.

Katika hatua nyingine muhimu, Naibu Mkurugenzi huyo alizindua rasmi kaulimbiu ya Muharram kwa mwaka 1448H/2026, inayosema: "Karbalaa ni njia ya uhuru wa kufikiri".

Kaulimbiu hiyo inalenga kuihamasisha jamii kujikita katika kutafakari kwa kina mchango wa Karbalaa katika kuimarisha fikra huru, kupinga ukandamizaji na kuijenga jamii inayozingatia haki, uadilifu na utu wa binadamu.

Hafla ya upandishaji wa bendera ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na kijamii, akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, pamoja na wageni wengine walioonesha mshikamano wao katika kuadhimisha mwezi wa maombolezo ya Sayyid al-Shuhadaa Imam Hussein (as).

Maoni yako

You are replying to: .
captcha